Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa NIRC Watembelea Bonde la Ulemo-Zinziligi-Belekese kwa ajili ya Uwekezaji wa Umwagiliaji




Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji (NIRC), Bw. Raymond Mndolwa, wametembelea Bonde la Ulemo-Zinziligi-Belekese, Wilayani Iramba Mkoani Singida kwa lengo la kuangalia namna ya kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kupata sehemu ya kujenga Bwawa, uchimbaji wa visima pamoja na miundombinu ya umwagiliaji katika eneo lenye ukubwa wa Hekta 43,000.




Miundombinu hiyo ikijengwa inatarajiwa kuhudumia wakazi wa Kata 6 ambazo ni Ulemo, Ndago, Mbelekese, Makulu, Kaselya na Kyengege.

Post a Comment

0 Comments