Balozi Stephen Mbundi akizungumza na Mkurugenzi wa AICC kuhusu Maboresho na Fursa za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia maswala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) Bi. Christine Mwakatobe.


Kikao kazi hicho kimefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa nchi za Afrika Mashariki unaoendelea katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.


Kikao kazi hicho kilijikita katika kuangalia namna bora ya kuibua na kutazama fursa mpya zenye tija na hivyo kutoa huduma bora na kuendelea kukiimarisha na kuvutia wateja wengi zaidi katika kituo hicho cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC.


Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa AICC Bi mwakatobe amemweleza Balozi Mbundi kuwa AICC inaendelea kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu na kuongeza kuwa wamejipanga kufanya maboresho makubwa ambayo yataleta tija na ufanisi kwa taasisi.


Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Balozi Mindi Kasiga na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Wateja wa AICC Bw. Assah Mwambene.

Post a Comment

0 Comments