NAIBU WAZIRI LONDO AKUTANA NA NAIBU WAZIRI KUTOKA UJERUMANI




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Kazi na Masuala ya Kijamii wa Ujerumani, Mhe. Kerstin Gríese jijini Dar Es Salaam Agosti 19, 2024.



Wakati wa mazungumzo yao wamejadili na kuahidi kuendeleza na kudumisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Ujerumani kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano katika elimu kwa kuanzisha programu za kubadilishana ujuzi kwa vijana wa Kitanzania.


Aidha Mheshimiwa Londo amemueleza Mhe. Kerstin Gríese changamoto ya ajira kwa vijana nchini kutokana na kuongezeka kwa wingi wahitimu wa elimu ya juu na kutoka taasisi nyingine ambao wanazidi soko la sasa la ajira, hivyo, amewaomba wadau wa Ujerumani kuja kuwekeza nchini ili kuzalisha ajira zaidi, na pia kuchukua vijana wa kitanzania wenye vigezo kwa fursa za ajira za nchini

Post a Comment

0 Comments