Matukio ya Kufana Katika Mahafali ya Shule ya Awali na Msingi Debla, Kahama.



Na Raymond Mihayo,Kahama

Katika sherehe za mahafali ya Shule ya awali na Msingi Debla zilizofanyika leo katika Mtaa wa Shunu, Kata ya Nyahanga, Manispaa ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, matukio mbalimbali yenye kuvutia yalishuhudiwa huku wageni waalikwa na wazazi wakijumuika kwa furaha. Shule hii maarufu, ambayo imejipatia sifa kutokana na utoaji bora wa elimu, iliandaa sherehe hiyo kwa lengo la kuwaaga wahitimu wa darasa la saba.


Mgeni rasmi, BeatusTesha ambaye pia ni Meneja wa Benkiya Equity Tawi la Kahama, alihudhuria na kushuhudia sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Bi Rashmi aliwasihi wahitimu kutambua thamani ya elimu waliyoipata na kuitumia vyema katika maisha yao ya baadaye. Alipongeza jitihada za walimu na wazazi katika kuleta maendeleo ya kielimu na kuimarisha nidhamu miongoni mwa wanafunzi.


Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili, nyimbo, na maigizo yaliyoandaliwa na wanafunzi. Pia, wahitimu walipata fursa ya kutoa shukrani zao kwa walimu wao kwa kuwaongoza kwa ufanisi katika safari yao ya elimu.


Sherehe hiyo ilihitimishwa kwa kugawa vyeti kwa wahitimu pamoja na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao. Furaha na bashasha zilitawala wakati wote wa sherehe, ikionyesha jinsi jamii ya Shunu ilivyo na mshikamano katika kuiinua elimu.


Katika mahafari hayo jumla ya wanafunzi wa awali 28 wanatarajia kuanza darasa la kwanza mwakani huku wanafunzi 19 wa darasa la saba wamehitimu elimu ya msingi

Post a Comment

0 Comments