MRADI WA SMART CITY ARUSHA WAPATA NONDO KUTOKA NIGERIA, ASKARI WALIOPATA MAFUNZO KUBORESHA MIRADI YA ULINZI KIDIGITALI TANZANIA





Na. Abel Paul, Abuja Nigeria.


Askari kutoka nchini Tanzania wamefika Makao Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini Nigeria ambapo wametumia ziara hiyo kujifunza masuala ya usalama na matumizi sahihi ya Tehama katika kuimarisha ulinzi huku washiriki wakihaidi kutumia mafunzo hayo kuboresha matumizi ya kidigitali katika ulinzi pindi watakapo rudi Nchini Tanzania.


Akiongea leo Julai 09,2024 Baada ya mafunzo hayo Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi amesema kuwa wamejifunza namna ya kudhibiti uhalifu kwa kutumia mifumo ya kidigitali ambayo inauwezo wa kutazama eneo lote la mji na askari kupata taarifa na kufika eneo la tukio kwa wakati.


SSP Georgina ameongeza kuwa tayari Nchini Tanzania mradi huo wa Smart City ushaanza na unaendelea katika jiji la Arusha ambapo amebainisha kuwa wanakwenda kuongeza utaalam walioupata Nchini Nigeria huku akiweka wazi kuwa vitu walivyoviona katika mafunzo yao yameonyesha kuwa Nchi hiyo imeendelea katika ulinzi kidigitali.


Kwa Upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamzi wa Polisi SACP Dkt Debora Magiligimba amesema lengo la ziara ya mafunzo hayo nikuona na kujifunza namna ambavyo Jeshi la Polisi Nchini Nigeria linafanya kazi huku akibainisha kuwa wamepata mambo mapya ambayo yanakwenda kuboresha utendaji wa kazi zao.


Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi amesema kuwa Jambo ambalo wamejifunza ni ufuatiliji wa kesi na uwekaji wa mahabusu katika vituo vya Polisi huku akibainisha kuwa mambo hayo walioyaona nchini Nigeria tayari Tanzania wameshayafanya kupitia maelekezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania na tume ya haki Jinai.


Mrakibu Mkuu wa Polisi Kutoka Nchini Nigeria CSP Abubakar Sadiki amesema kuwa amefurahi kutembelewa na askari kutoka Nchini Tanzania katika kituo hicho ambacho askari hao walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali wanayofanya Jeshi hilo Nchini humo.

Post a Comment

0 Comments