Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 02, 2024 ameweka jiwe la msingi la jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyangh’hwale ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 85.
Akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo ambapo mpaka sasa limegharimu shilingi bilioni 3.7, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha majengo ya utawala kwenye halmashauri zetu “Lengo la Rais Dkt. Samia ni kuona wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao”.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakuu wa Idara na watumishi wengine kwenye Halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu mkubwa katika kuwahudumia wananchi “Wananchi wana matumaini makubwa na Serikali yao, wahudumieni na mtatue kero zao”
Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo mkoani Geita kwa ziara ya kikazi.
0 Comments