Sheikh Omary Damka akiwahusia wauumini wa dini ya kiislamu katika swala ya Eid El Adh-ha
NA NEEMA NKUMBI -NKUMBI MEDIA KAHAMA
Sheikh wa Wilaya ya Kahama Sheikh Omary Damka amewataka waumini wa dini ya kiislamu kutumia fursa ya uhai walionao kuwajengea maadili mema vijana wao kwani vijana wao ni Taifa la kesho endapo wasipowajengea maadili mema ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika hali mbaya zaidi
Amesema hayo juni 17, 2024 katika swala ya Eid El Adh-ha iliyoswaliwa katika uwanja wa halmashauri ya manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Amri Kalokola ambaye ni muumini wa dini hiyo amesema wazazi wajitambue na kuwapeleka watoto katika hule zinazofundisha imani wajifunzemisingi ya dini na kuheshimu wazazi.
Mwasiti Issa amewataka wazazi wenzake kujitahidi katika malezi na kuwapeleka watoto madrasa waweze kupata maadili ya Mwenyezi Mungu pia waepuke kuwapa simu maana katika simu kuna vitu ambavyo ni tofauti na umri wao.
Naye Tausi Kilonge amesema watoto ni wengi mtaani wanaokota vyuma hali inayopelekea kuwa wadokozi hivyo amewataka wazazi wenzake kuwajali watoto wao
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Eid El Adh-ha katika uwanja wa halmashauri ya manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
0 Comments