SERIKALI YA MTAA WA MHONGOLO IMEKABIDHI MADAWATI 50 KATIKA SHULE YA MSINGI MHONGOLO

 





NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL-KAHAMA




Picha ya miti iliyokatwa kwa ajili ya kutengeneza madawati


Upandaji miti unafaida kubwa kwa binadamu licha ya kupata hewa safi pamoja na matunda shule ya Msingi Mhongolo imejipatia madawati hamsini na meza mbili za waalimu baada ya kukata miti 29 waliyoipanda katika shule hiyo


Mwenyekiti wa mtaa wa Mhongolo Emanuel Nangali amesema madawadi hayo yamepatikana kutokana na miti iliyovunwa katika eneo la shule hiyo ambapo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa madawati hali ambayo baadhi ya wanafunzi walikuwa wanakaa chini darasani kwa kukosa madawati.


Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa wamekuwa na ushirikiano baina ya kamati ya shule , serikali ya mtaa na walimu katika masuala mbalimbali ya maendeleo hivyo ushirikiano wao unalenga kuongeza ufalu mzuri wa wanafunzi.


Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa kamati ya shule Clement Masonga amesema waliiomba serikali ya Mtaa kibali cha kukata miti ili kutengeneza madawati hayo baada ya kukata miti hiyo walipata mtu ambaye walikubaliama awatendenezee madawati na wao wachukue miti hiyo.




Aidha Mkuu wa shule ya Mhongolo Enest Peter ameipongeza serikali ya mtaa pamoja na Kamati ya shule kwa kuwezesha zoezi hilo kukamilika kwani shule hiyo ina wanafunzi elfu mbili mia tano pia ameiomba serikali kuongeza idadi ya walimu kwani kuna waalimu thelathini na tano.


Mwalimu Enest ameongeza kuwa kuna uhaba wa matundu ya choo kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo hivyo walikaa kikao na wazazi, Kamati ya shule pamoja na serikali ya Mtaa wamekubaliana kuchangia mchango wa shilingi elfu tatu na sasa wameanza kuchimba shimo la choo hivyo amewataka wazazi ambao bado hawajamaliza michango hiyo wamalizie ili choo kikamilike mapema.



Mwenyekiti wa mtaa wa Mhongolo akizungumza na Huheso Digital


Baadhi ya miti inayopatikana katika shule ya Mhongolo



Mkuu wa shule aliyevaa miwani na pembeni ni mwenyekiti wa mtaa wakikabidhiwa madawati na aliyeyatengeneza

Post a Comment

0 Comments