FAMILIA YA MTOTO ASIMWE YAFARIJIWA NA MR. MANGURUWE




Mkurugenzi kutoka kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero Dodoma Simon Mnkondya maarufu Mr. Manguruwe Juni 23,2024 amefanya safari kutokea Dodoma kuelekea Muleba mkoani Kagera katika kijiji cha Bulamula Kata ya Kamachumu yalikotokea mauaji ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath (2) kwa ajili ya kuipa pole familia ya Mama wa Marehemu Asimwe.


Hivi karibuni Mwili wa mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath ambaye alichukuliwa na watu wasiofahamika nyumbani kwao katika kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu ulikutwa ukiwa umetupwa kwenye karavati na kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili katika kijiji cha Marere kata ya Ruhanga wilaya ya Muleba.








Post a Comment

0 Comments