ELIMU YA FEDHA IMETOLEWA KWA WANANCHI WA KAHAMA



Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, wamepata fursa ya kupewa mafunzo ya elimu ya fedha na timu ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), washiriki wa mafuzo hayo walipata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kifedha ikiwemo utunzaji wa fedha binafsi, uwekaji wa akiba, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha (vikoba) na kuhifadhi fedha za vikundi hivyo benki, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kuhusu mikopo na uwekezaji pamoja na kuandaa maisha ya uzeeni na kustaafu.


Wizara ya fedha inaendelea na programu ya kutoa elimu ya fedha kwa umma nchi nzima ambapo baadhi ya mikoa iliyofikiwa ni pamoja na mkoa wa Manyara, Tabora, Simiyu, Singida, Kagera, Shinyanga huku zoezi hilo likiwa ni endelevu lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata uelewa kuhusu huduma za fedha ili waweze kuepuka mikopo umiza.

Post a Comment

0 Comments