NA NEEMA NKUMBI -KAHAMA
Jeshi la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limesema limejipanga kuendelea kutokomeza vitendo viovu vinanvyoendelea kujitokeza katika jamii
Hayo yamesemwa katika kikao kazi kilichofanyika katika Bwalo la Polisi kiliwakutanisha wafanyakazi wa Jeshi la Polisi Pamoja na wake zao na waume zao, Viongozi wa Dini na wadau mbali mbali, kikao kilichokuwa na lengo la kuendelea kuwajengea uwezo Maaskari wa Jeshi la Polisi Pamoja na kuangalia changamoto zinazoikabili jamii Wilayani hapo
Pamoja na hayo baadhi ya wadau akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Kahama Bw Thomas Myonga amekemea vitendo vya baadhi ya maaskari Polisi kujihusisha na suala la rushwa hali inayopelekea kukosekana kwa usawa na haki katika jamii hivyo kujenga matabaka katika jamii
''...Unalipa ada ya mtoto kwa pesa ya rushwa, umemmaliza na mimi niseme unaweza ukamkuta Askari ni mlevi wa kupindukia na ana tabia za ovyo, fuatilia historia ya namna alivyosomesha na alipotokea unaweza kukuta amesomeshwa kupitia mambo ya ajabu’’ Amesema Myonga
Kwa umuhimu wa Viongozi wa dini katika kikao hiki Sheikh Mkuu wa BAKWATA Wilaya ya Kahama Sheikh Adam Damka alikuwa miongoni mwa walioalikwa kutoa mawaidha ambapo amewaasa Maaskari kuutumikia wito huo ambao wamepewa na Mwnyezi Mungu mwenyewe
" Kwa kuwa mmepata neema hii, hamna budi kulitumikia hili kwa kutambua kuwa ni wito ambao mmepewa na Mwenyezi Mungu hivyo mjifunze kuwatumikia wananchi kwa haki mkimkumbuka Mwenyezi Mungu huku mkijipamba na maadili yenu ya kazi ikiwa ni Pamoja na nidhamu katika kazi yenu’’
Askofu wa Jimbo Katoriki la Kahama Mjini Josephati Ndizeye katika hotuba yake yeye amesema ili waweze kuitumikia jamii kwa haki na usawa ni lazima wajifunze jambo jipya kila siku ambapo sambamba na hilo amewapongeza Polisi kwa kazi ambayo wanaendelea kuifanya kwa kuhakikisha amani na usalama katika mazingira yetu
‘’ Hatuwezi kuwa na Amani katika maeneo yetu nab ado tukaona mabaya ya Jeshi la Polisi tukasahau yale mazuri yao, inawezekana wapo wengi kati yao ambaoo wanafanya mabaya lakini hawa wezi kuwa wote, licha ya hayo mazuri lakini bado kuna changamoto mbali mbali kama vibaka, wavuta bangi, mambo ya ulawiti bado yanazidi kuongezeka na bahati mbaya zaidi Kahama imepata sifa mbaya ya kujihusisha na biashara ya binadamu si kwa Kahama tuu bali hata nje ya Kahama wanalifahamu hilo’’
Katika mahojiano kati ya waandishi wa Habari na Mkuu wa Jeshi La Polisi Manispaa ya Kahama SSP Mtaju Msiba Mayombo baada na hafla hiyo amesema kuwa kikao kazi hicho kililenga kuonesha jamii kuwa Jeshi la Polisi liko wazi na ni sehemu ya Jamii ya Watanzania
‘’ ni kweli kuwepo kwa mabadiliko ya sayansi na Teknolojia kunakuja na tabia ambazo hazikuwepo katika jamii na hatukuzitegemea lakini jeshi la Polisi tumejipanga kushirikiana na Mamlaka nyingine zinazohusika ili kama siyo kutokomeza kabisa basi kupunguza vitendo hivyo katika jamii’’ Amesema Mtaju
Askofu wa Jimbo Katoriki la Kahama Mjini Josephati Ndizeye katikati
0 Comments